Burudani

Christian Bella atangaza nafasi za kazi

Msanii wa muziki Bongo, Christian Bella ametangaza kuanza kutoa nafasi kwa vijana katika band ya Malaika.

Muimbaji huyo ambaye anatamba na ngoma ‘Shuga Shuga’, ameimbia The Base, ITV kuwa katika kuongeza nguvu kwenye team yake anatoa fursa kwa vijana wenye uwezo wa kuimba live, kupiga gita na kinanda.

“Nahitaji pia kuboresha team, kijana yeyote mwenye talent ya kuimba live kuna fursa ya kazi kwangu, namkaribisha, awe mpiga gita, awe mpiga kinanda anicheki tu kwenye Instagram yangu” amesema.

Bella ameongeza kuwa si kwamba sasa hana wa kufanya nao kazi ila anachotoka ni kuiboresha zaidi Malaika Music Band.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents