Burudani

Christiana Bella: Kama sio Godfather, ntaenda na Adam Juma kushoot video South

Christian Bella ana option mbili ya kushoot video ya wimbo wake ujao ‘Nashindwa’ nchini Afrika Kusini – kumtumia Godfather au kusafiri na Adam Juma.

Christian Bella

Bella ameiambia Bongo5 kuwa kampuni aliyoipa kazi hiyo ikishindwa kufanya kazi kwa wakati itambidi aAchane nao na kumpa Adam Juma kutokana na uhitaji wa kazi hiyo kwa haraka.

“Ngoma pamoja na video nataka kutoa mwezi huu au ujao au wa tatu mwanzoni. Kuna watu ambao nimesaini nao mkataba ambao tumekubaliana nao tukafanye video kwa Godfather lakini wakinichelewesha mimi kwa sababu na haraka ya kutoa namchukua Adam Juma naenda nae South,” amesema Bella.

“Mpaka sasa dalili ni Godfather lakini mimi mwenyewe nina plan B. Unajua katika maisha usitegemee mtu huyo ni mkataba ambao nimesaini na kampuni moja hivi lakini wakinichelewesha namchukua Adam naenda naye.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents