AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Chuki inasababisha kushuka kwa Bongo Movie – Shamsa Ford

Msanii wa filamu Bongo, Shamsa Ford amedai kuwa chuki inafanya tasnia hiyo kushuka.

Muigizaji huyo amesema kitu hicho kimefanya wasanii wengi kukoseshana dili ambazo zingeweza kutangaza tasnia hiyo nje ya nchi.

“Ni kweli kwa sababu Bongo Movie wengi hatupendani, hasa wanawake hatupendi kuwa mabalozi wazuri kwa wanawake wengine, kwa hiyo mwisho wa siku zile chuki zinafanya isiendelee,” amesema Shamsa Ford.

“Lets say mtu anatoka nje anataka kufanya kazi na Shamsa, unaanza kuponda usifanye naye kazi, mwisho wa siku dili linaondoka wakati ngingefanya ningewakilisha wasanii wa Bongo na pia Tanzania, so chuki inasababisha kushuka kwa Bongo Movie,” amesisitiza.

Mwaka 2014 Shamsa Ford kupitia filamu yake ‘Chausiku’ aliweza kufikia rekodi ya mauzo ya filamu iliyowekwa na filamu ya mwisho ya marehenu Steven Kanumba, ‘Love and Power’, rekondi ya mauzo hayo ni kwa mujibu wa Steps Entertainment.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW