Tia Kitu. Pata Vituuz!

Chuo cha Afya Kigamboni chaiomba Serikali kutengeneza Sanitizer za Corona baada ya kupanda bei na kuadimika madukani – Video

Chuo cha Afya Kigamboni chaiomba Serikali kutengeneza Sanitizer za Corona baada ya kupanda bei na kuadimika madukani - Video

Chuo cha Afya cha City College kilichopo Kigamboni jijini Dar Es Salaam kimeiomba Serikali nafsi ya kutengeneza vimiminika aina ya Sanitizer kwa ajili ya kujikinga na virusi vya Corona baada ya kusikika kupanda bei na kupungua kwa kasi madukani.

Kupitia kwa Mkurugenzi wa Chuo hicho Dkt. Shabani Mwanga ameeleza kuwa Chuo hicho kinachojihusisha na masuala ya kiafya kina uwezo mkubwa wa kutengeneza vimiminika hivyo kwa ubora zaidi na kuweza kuisaidia jamii ya Kitanzania kutokana na hali ilivyo kwa sasa baada ya vimiminika hivyo kupanda bei na kupungua madukani.

Kupitia Waziri mwenye dhamana Mh. Ummy mwalimu Chuo hicho kimeomba nafasi hiyo ya kutengeneza Sanitizer kwa waamini kuwa kwa wataalamu na maabara waliyonayo pamoja na vifaa vinavyopatikana chuoni hapo wanauwezo wa kuvitengeneza kwa kiasi kikubwa na hatimaye kuvisambaza katika jamii kwa bei nafuu sana.

Mbali na hivyo wanafunzi wa Chuo hicho wameeleza na kuwaasa wanafunzi wenzao baada ya vyuo vyote kutangazwa na Mh. Waziri Mkuu kufungwa kuwa isiwe ni nafasi kwa wao kwenda kubweteka bali watumie nafasi hii ya siku 30 walizonazo mtaani kuelemisha jamii kuhusu namna ya kujikinga na Corona.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW