Habari

Chuo kikuu cha Dodoma kuzalisha umeme wa megawati 55 kwa kutumia jua

Chuo kikuu cha Dodoma kinatarajia kuzalisha umeme wa jua utakaoweza kuzalisha megawati 50.

home+sub+1+pix

Mradi huo mkubwa unatarajiwa kujengwa na kuwa mkubwa kuliko chuo chochote kuwahi kujenga ndani ya eneo la chuo duniani. Megawati hizo zitatumika kwa kuanzia kusambaza umeme kwenye mabweni, madarasa ya kufundishia, sehemu za kufanyia tafiti na eneo la madawa au huduma za afya.

Unatarajiwa kukamilika wote hadi kufikia mwaka 2016 na unatarajiwa kuzalisha umeme wa kusaidia sehemu ya kati ya mkoa wa Dodoma. Mpango huo wa chuo cha Dodoma ni mkakati mahususi wa kuwa sehemu inayoonyesha ufanisi wa matumizi bora za nguvu ya jua na mbadala wa nguvu ya umeme.

Mpango huo ni kuhakikisha Tanzania inazalisha wafanyakazi waliofunzwa vizuri, wanasayansi wanaofanya shughuli za kitafiti, na wajasiriamali watakaongoza bara la Afrika katika kutumia nguvu ya umeme isiyochafua mazingira.

Kukamilisha malengo yao wameingia mkataba na chuo kikuu cha Ohio ambacho kinaheshimika kutokana na tafiti mbalimbali duniani kwa mambo ya chakula, maji, umeme na afya.

Wakati wa uzinduzi wa mradi huo mkubwa wa kutumia nguvu ya jua katika taasisi ya nguvu ya umeme mbadala na yenye uhakika, mkuu wa kitengo cha taasisi ya maji kutoka chuo kikuu cha Ohio alisema kuwa amefurahi kwamba mradi huo unaenda kuwa halisi.

Wakati huo huo mpango huo unaonesha kasi ya kupunguza mgao wa umeme ambao umekuwa sugu katika nchini.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents