Habari

Chuo kikuu cha Harvard chatangaza fellowship ya Nas ‘Nasir Jones Hip-Hop Fellowship’

Rapper mkongwe wa Marekani, Nas amepewa heshima na chuo kikuu maarufu duniani cha Havard ya kuanzishiwa fellowship yenye jina lake.

66255ec6bf7eaff7b526549d03d3de02

Chuo kikuu hicho kimeanzisha fellowship hiyo kwa heshima ya rapper huyo ambaye amekuwa na career yenye mafanikio kwa zaidi ya miongo miwili. Idara ya W.E.B. Du Bois ya chuo kikuu cha Harvard imeitangaza ‘Nasir Jones Hip-Hop Fellowship’ jana ikiwa na lengo la kutoka fursa kwa wanafunzi na wasanii watakaochaguliwa kuonesha kuwa elimu ni nguvu ya kweli.

“I am immensely over-the-top excited about the Nasir Jones Hip-Hop Fellowship at Harvard. From Queens, NY to true cultural academia. My hopes are that greed for knowledge, art, self-determination and expression go a long way. It is a true honor to have my name attached to so much hard work, alongside great names like Henry Louis Gates, Jr. and W.E.B. Du Bois and to such a prestigious and historical institution, and all in the name of the music I grew to be a part of,” alisema Nas baada ya kupewa heshima hiyo.

Fellowship hiyo itakuwa ikitafuta miradi ya kiubunifu kutoka kwa wasomi na wasanii wanaojihusisha na utamaduni wa Hip Hop. Itawakilisha pia mchango wa mtu wa kiubunifu na kisomi kwa hip-hop.

Miradi hiyo binafsi ni pamoja maandishi, vipande vya performance, kazi za albam, mipango ya mitaala, utafiti wa kumbukumbu na maandalizi ya maenesho ya sanaa. Wanafunzi watakaopata fellowship hiyo watachaguliwa na kamati inayoundwa na kitivo cha Harvard.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents