Tupo Nawe

Chupu chupu zichapwe Anthony Joshua vs Jarrell Miller, AJ aahidi kumfanyia unyama mpinzani wake ulingoni

Bingwa wa uzito wa juu duniani, Anthony Joshua ameahidi kumchakaza mpinzani wake Jarrell Miller baada ya wawili hao kukutana na vyombo vya habari hii leo siku ya Jumatatu.

Wawili hao wamezungumza na vyombo vya habari kuelekea pambano lao litakalo pigwa Madison Square Garden huko New York siku ya Jumamosi ya Junu 1.

AJ atashuka ulingoni kutetea mikanda yake ya IBF, WBA na WBO dhidi ya Mmarekani huyo.

”Sitakuwa nikubwa cha kufanya kwenye uso wake, lakini nitakuwa daktari wake wa upasuaji, ninaenda kuutengena uso na mwili wake,” amesema Joshua huku akionekana mtu mwenye hasira.

”Hiki ndiyo kitu pekee ninachokifahamu hivyo ndivyo ninavyofanya siku zote. Ninachokifahamu mimi ni kuwapiga tu.”

The American refused to acknowledge the champion when he made his way to the top table

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW