Burudani

Ciara anusurika kifo kwenye ajali ya gari Los Angeles

Ciara amenusurika kifo kwenye ajali ya gari iliyotokea Ijumaa hii mjini Los Angeles.

Ajali hiyo imetokea wakati mrembo huyo alikuwa akiendesha gari lake aina ya Mercedes-Benz G-Wagen yenye rangi nyeupe ndipo aligongana na gari jingine aina ya Volvo SUV kwenye upande kiti cha abiria.


Ciara akiwa nje ya gari lake baada ya kupata ajali

Japo Ciara alidaiwa kuumia kifuani lakini kwa mujibu wa mumewe Russell Wilson kupitia mtandao wa Twitter amesema mama na mtoto wako salama.

“Momma Wilson & Baby Wilson are feeling great! God is good! ????????????????????????,” ameandika Russell kwenye mtandao huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents