Burudani

Cindy Rulz adai tuzo za KTMA zimewatenga rappers wa kike

Rapper Corrine Mary a.k.a Cindy Rulz amedai tuzo za Kilimanjaro haziwapi support rappers wa kike kutokana na kukosekana kwa kipengele cha msanii wa hip hop wa kike.

BZqQZd-CcAAQYDO.jpg large

“Mfano huwezi ukaniweka category moja na akina Recho au Linah sijui Dayna itakuwa tofauti, ndio maana ukiona tuzo za watu wa nje huwezi kuona Nick Minaj anapangwa pamoja na watu kama akina Rihanna maybe kama kwenye Videos of the year,” Cindy alikiambia kipindi cha Bomba Base Show cha Bomba FM Radio, Mbeya.

“Lakini kungekuwepo na kipengele cha Female Rappers kipengele ambacho female rappers tunashindanishwa sisi wenyewe kama Chiku Keto, Cindy Rulz, Witness au Stosh, naona tuzo zetu hazipo katika kusapoti female rappers. Sijawahi kuona yaani Female Rappers wasanii wa zamani kama akina Zay B, Sister P na Rah P wakitunzwa na hizi tuzo kutokana na kukosa hicho kipengele.”

Rapper huyo aliongeza kuwa utaratibu wa kuachia ngoma zake mpya ni tofauti na wasanii wengine kutokana na wengi wao ku-target kipindi cha utoaji wa tuzo.

“Well to be honest sijawahi kufanya kazi zangu za muziki nikaweka nguvu sana kwamba nafanya hii ngoma ili itue kwenye Kili Music Awards hapana, nakuwa natengeneza muziki mzuri kwaajili ya kuwafurahisha mashabiki, ukiwa unatengeneza muziki kwaajili ya tuzo aaaah, hiyo dizaini inakuwa kazi sana kwa sababu incase imetokea bahati mbaya hujawa nominated unaweza ukadata, mimi natengeneza muziki mzuri na tuzo iwe tu kama bonus, yeah kama jina lilivyo nitunzwe tu kwa sababu nafanya kitu kizuri,” alisema.

“Nipate tuzo nisipate tuzo bado nitaendelea ku-push muziki wangu sehemu ambayo kwangu ningependa uweze kufika, kama ikitokea bahati nzuri nimekuwa nominated na nikashinda yote heri, lakini focus yangu haipo hapo focus yangu nikutengeneza muziki mzuri hits song after hits song, good music watu waupende tuendelee kusonga na maisha kama vitu vingine.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents