Burudani

Cjamoker wa SSK apata nafuu

Moja ya member wa kundi la muziki wa Hip Hop Bongo SSK, Oscar Mwailunga a.k.a Cjamoker aliyekuwa amelazwa hospitali ya Muhimbili chini ya uangalizi maalumu anaendelea vizuri.

Cjamoker

Kupitia mtandao wa Instagram rapa huyo ameposti kujulisha mashabiki zake na wadau waliomsapoti.

“Napenda kuwashukuru watu wote waliochuku muda wao kunijulia hali na pia kuchangia katika zoezi la kuhakikisha ninapata matibabu,” ameandika rapa huyo

Aliongeza kwa kuandika ” Mmenionesha upendo na fadhila ya hali ya juu, na hakuna namna yoyote ninayoweza kuwalipa. Mliipa familia yangu faraja na pia maombi na sala zenu zilinipa nguvu ya kuweza kupigania maisha yangu wakati nipo hoi na sijitambui.”

Rapa huyo kwa sasa anaendelea vizuri ila bado amelezwa Hospital ya taifa ya Muhimbili hospitali, wodi ya Kibasila, Chumba namba 13.

Hata hivyo moja ya member wa kundi hilo P the Mc ameongea na Bongo5 kuhusu hali ya rapa huyo.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents