MichezoUncategorized

Cleveland Cavaliers wapata ushindi wa kwanza dhidi ya Boston Celtics

Ikiwa ni mchezo wa tatu kati ya michezo saba ya Conference Final zone ya Easter,Alfajiri ya kuamkia leo Cleveland Cavaliers wamefanikiwa kupata ushindi wa kwanza kwa kuwafunga wapinzani wao Boston Celtics kwa vikapu 116 kwa 86.

Katika michezo miwili iliyopita Boston Celtics walifanikiwa kushinda michezo yote miwili hivyo mchezo wa jana umefanya series kuwa 2:1 Boston wakishinda michezo miwili na Cavs wakishinda mchezo mmoja na kubakiwa na michezo minne aweze kujulikana mbabe wa Eastern Conference atakaekutana na mbabe mwingine kutoka zone ya Western kati ya Golden State Warriors dhidi ya Houston Rockets mchezo ukitarajiwa kupigwa Alfajiri ya Mei 21.

Lakini katika mchezo uliochezwa alfajiri ya kuamkia leo Lebron James au ukipenda muite KingJames alifanikiwa kuibeba Timu yake kwa mara nyingine tena huku akifunga vikapu 27,Rebounds 4 na Assists 12 akisaidiana vizuri kabisa na mchezaji mwenzake kutoka Cavs simwingine bali ni Kevin Love aliyefunga vikapu 13 na kufanya Rebounds 14 katika mchezo huo.

kocha mkuu wa Cleveland Cavaliers Bwana Tyron Lue amempongeza Lebron na kusema anaimani nae mapema baada ya mchezo huo kumalizika.Imeandaliwa na Ally jei

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents