Habari

Clinton na Trump wawabwaga wapinzani wao New York

Zaidi ya nusu ya kura zilizohesabiwa katika uchaguzi wa awali wa vyama katika kinyang’anyoro cha urais nchini Marekani katika mji wa New york, zinaonesha kwamba Donald Trump na Hillary Clinton wamepata ushindi mkubwa zaidi.

160420034108_cn_trump_clinton_new_york_combo_512x288_reuters_nocredit

Hillary Clinton ambaye amemshinda mpinzani wake Bernie Sanders kwa ushindi mkubwa ameeleza katika hotuba yake kuwa ushindi wa chama chake cha Democratic umeweza kuwaunganisha zaidi wapinzani wake kuwa wamoja.

Hata hivyo New York inatajwa kuwa ngome nyingine ya Donald Trump,ambapo Cruz yeye hesabu za kura zake zimeonekana kugoma mapema kabisa katika chama chake cha Republican .

Wakati Hillary Clinton amemshinda mpinzani wake Bernie Sanders kwa ushindi mkubwa, amewaambia wapinzani wake kuwa kuna la ziada linalowafanya wawe wamoja zaidi ya kuwagawa.

Source: BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents