Burudani

Clouds FM Yaandaa Street Bash Club Billicanas Jumapili Kusherehekea Miaka 13

Wafanyakazi wa Clouds Fm.
Katika kusherehekea Birthday ya Miaka 13 tangu kuanzishwa kwake, kituo cha Radio cha Clouds FM kitafanya Street Bash kwa event kali ambayo inatarajiwa siku ya Jumapili ya wikiendi hii, ikikutanisha wasanii mbali mbali wa kizazi kipya.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa watangazaji wa Radio hiyo wasanii mbali mbali wakiongozwa na mshindi wa tuzo ya Channel O kupitia kipengele cha “Most Gifted African East Video Of The Year” AY atakuwepo kwa mara ya kwanza kukupa kile kilichopelekea ubora wake kutambuliwa kimataifa.
Ratiba ya tukio hilo inaonyesha event hiyo imepangwa katika setting tatu ambapo kutakuwa na Live performance shoo katika parking ya club Billicanas kwa mtindo wa Street Bash na pia kutakuwa na DV J Muli B, DVj Bulla na DJ Ibra. performance ndani ya ukumbi wa ndani wa Club hiyo, kabla ya kuhitimisha na party nyingine katika usiku huo huo ambyo itakuwa upande wa Club Much More.
Zaidi ya wasanii kumi na tano wataimba katika shoo ambayo imewekwa viingilio vya shilingi 15,000/ kwa mtu atakayetaka kuona na ku access pande ama setting zote tatu na shilling 10,000/ kwa wale watakaotaka kuona Street Bash tu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents