Habari

Club 327 yaendana na hali ya uchumi wa Tz kutokana na bei ya vinywaji


Baada ya kukuletea habari ya uzinduzi wa Club mpya ya usiku Club 327, Mkurugenzi Mtendaji wa Club hiyo mpya, Bwana Lawrence Kadri leo asubuhi ameitambulisha rasmi Club hiyo kwa waandishi wa habari na kuwaeleza machache kuhusiana na kiota hicho cha burudani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar-Es-Salaam, Bwana Lawrence alisema Club yake ni maalumu kwa ajili ya watu wanaotaka ku party ki tofauti kwa sababu kwanza wamezingatia suala la bei ya vinywaji na pia mandhari ya club ili kuwapatia wateja wa burudani chaguo la kipekee katika suala la matumizi na uchaguzi
Bwana Lawrence alisema Club yake ina jumla ya sehemu kuu mbili yaani ukumbi wa chini na ule wa juu, ambapo ukumbi wa juu una vyumba maalumu vitatu kwa ajili ya VIP ambapo kwa wale watakaotaka exclusivity watalipa kiasi cha shilingi laki tatu na kupata moja kayi ya chupa ya Moet Champaigne, Hennessy na Belverede Vodka ambayo ni sehemu ya malipo hayo.
“Kama unavyoona vyumba hivi vina ukubwa tofauti kwa mfano chumba cha Hennessy kina uwezo wa kuchukua watu watano, Moet Kina uwezo wa kuchukua watu 6 na Belvered Vodka kinachukua watu nane ambapo vyumba vyote vina friji mbili ndogo ndogo, choo cha ndani, TV sets kwa ajili ya kuburudika na pia kufuatilia kinachoendelea ndani ya Club”.
Akiendelea kufafanua Mkurugenzi huyo alisema kutakuwa na wahudumu kwa ajili ya kukupa usaidizi kwa mahitaji madogo madogo ya kawaida, kwa mfano kama unataka vocha, vinywaji, chakula wao watakuwepo kukupa huduma hiyo.
Aliendelea kusema, Club hiyo itaanza kutoa huduma zake kwa siku za kawaida kwa mtindo wa happy hours ambapo milango itakuwa wazi kuanzia saa kumi na moja mpaka usiku na kuendelea. Vinywaji katika Club hiyo ya 327 vitaanzia kwa bei ya shilingi 3000 kwa bia za Kitanzania na shilingi 5000 kwa bia za nje. Bei hizi zimezingatia hali halisi ya kiuchumi kwa walio wengi ili wapate nafasi ya kuburudika kama watu wengine.
Akielezea historia yake fupi katika upande wa biashara ya madisko bwana Lawrence alisema yeye ana uzoefu mkubwa na imekuwa ndoto yake ya siku nyingi kumiliki Club na kuendesha kitu ambacho anaamini anakiweza,
Tunamnukuu “ mimi nina uzoefu katika shughuli za Club kwani kwanza mi ni Dj ambaye nilipiga enzi za Club Mbowe( sasa hivi Billicanas) kabla haijafungwa kupisha kubomolewa na kutengenezwa upya na kuitwa Cluub Billicanas.
Ukiachilia Club hii nimepiga pia na Dj Supa Deo katika Disko moja lililokuwa linaitwa Vision na pia nimepiga pale Ymca nimeendesha Club maarufu ya usiku ya California Dreamers kabla ya mmiliki wa eneo lile kufariki kwa miaka mitano na ndipo nilipopata wazo la kutimiza ndoto zangu la kuanzisha kitu chake mwenyewe.
Bwana Lawrence alimalizia kwa kusema viingilio kwa siku za kawaida ni shilingi elfu kumi na wikiendi kwa maana ya ijumaa, jumaosi na jumapili ambapo bei itakuwa ni shilingi elfu 20 katika ukumbi wa chini na elfu 30 katika ukumbi wa juu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents