Michezo

Club ya Azam yalazimishwa sare na AS FAR Rabat ya Morocco

Club ya Azam Fc ya Tanzania imelazimishwa sare ya bila kufungana jioni hii na AS FAR Rabat ya Morocco katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Tatu, Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

AZAM FC1
Matokeo hayo yanaifanya Azam iwe na mtihani mgumu katika mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo Morocco, wakitakiwa lazima kushinda au kutoa sare ya mabao ili kufuzu.

Pamoja na sare hiyo, Azam watakumbuka sana mabao matatu ya wazi waliyokosa kupitia kwa washambuliaji wao wa pembeni, Kipre Herman Tchetche mawili na Khamis Mcha ‘Vialli’ moja,Kipre aligongesha mwamba mashuti mawili katika dakika za 51 pembeni kushoto katikati na dakika ya 90 mwamba wa juu katikati baada ya jitihada za kuwatoka mabeki wa AS FAR Rabat.

Khamis Mcha naye alimtoka vizuri beki wa pembeni wa AS FAR Rabat dakika ya 52 lakini akapiga nje shuti lake.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Emile Fred wa Shelisheli, aliyesaidiwa na nduguze Steve Maire na Jean Ernesta pembeni, kipindi cha kwanza Azam walionekana kucheza kwa tahadhari zaidi na kufanya mashambulizi ya kushitukiza ila hayakuzaa matunda.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents