Burudani

CMB Prezzo ajibu tuhuma za matumizi ya madawa ya kulevya, asema hayo ni ‘malipo ya ustaa’

Kauli ya RapCellency CMB Prezzo the president inaoana na moja ya nyimbo za rapper wa River Camp, Bonta ‘Mti wenye matunda’. Prezzo amejibu madai yaliyotolewa hivi karibuni na aliyekuwa mke wake kuwa, amekuwa akitumia madawa ya kulevya na kushindwa kuilea familia na kuendekeza uzinzi na ulevi wa pombe.

Kupitia kipindi cha TV Str8 UP Live Jumamosi iliyopita, Jackson Ngechu Makini amedai kuwa mashambulizi yote hayo anayapata kwasababu tu yeye ni Prezzo, akimaanisha Prezzo ni staa ila kama angekuwa ni mtu wa kawaida tu (kwa kutumia jina lake la Ngechu) basi angekuwa anapitwa kama mti wenye maembe mabichi.

Akikanusha juu ya madai ya mke wake wa zamani kuhusu matumizi ya madawa ya kulevya alisema “Haiwezekani mtumiaji wa madawa ya kulevya aweze kusurvive kwa miezi mitatu bila kutumia madawa”, Kama akili yako iko sharp najua utakuwa umemwelewa!

Amemaanisha aliweza kukaa katika jumba la Big Brother ‘Star Game’ mwaka jana mwa muda wote mpaka fainali kitu ambacho mtumiaji wa madawa hawezi.

Kupitia kipindi hicho Prezzo licha ya kukana habari hizo aliweza pia kutoa ushauri kwa watu wote kuwa madawa si mazuri kwao na afya zao na yanazuia mafanikio “Drugs are not good for you and your health. Drugs limit success”.

Pia Prezzo Aliuonya umma na kuacha kueneza uvumi wa uongo juu yake na kuongeza usemi mwingine wa kujigamba “People say the sky is the limit, I believe that the sky is just the beginning point.”

Katika interview hiyo alikuwa na yule yule, unadhani nani? Ndio Huddah Manroe ambaye alikuwa akihojiwa katika show hiyo ya Live. Hapa The president, hapa The boss lady, kinachofuata malizia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents