Burudani

Comment iliyomchefua Aslay Instagram

Msanii wa muziki Bongo, Aslay amefunguka kuhusu comment zilizowahi kumchefua katika mtandao wa Instagram.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Natamba’ ameiambia Times Fm kuwa comment hizo alikutana nazo kipindi mama yake mzazi amefariki na yeye kwenda kwenye show.

“Comment ambayo siwezi kuisahu ni pale mama yangu alipofariki nikaenda kufanya show, nakumbuka ya CCM watu wanitukana sana, comment nyingi matusi,” amesema Aslay.

Hata hivyo katika hatua nyingine ameeleza kuwa hayupo tayari kuuza akauti yake ya Instagram kwa bei yoyote ile kwa sababu anaitengemea katika kutangaza muziki wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents