Michezo

Confederation Cup 2017: Ujerumani na Chile ngoma nzito, Cameroon na Australia wachungulia shimo

Alhamisi hii michuano ya hatua ya makundi ya kombe la mabara katika ngazi ya timu za taifa imeendelea tena kutimua vumbi huko nchini Urusi.

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa katika majira ya jioni kwenye uwanja wa Saint Petersburg, Cameroon walitoka suluhu ya kufungana kwa bao 1-1 na timu ya taifa ya Australia. Goli la Cameroon lilifungwa na Zambo Anguissa dakika ya 45, lakini kwenye dakika ya 60 mchezaji Milligan aliisawazishia Australia na kufanya matokeo ya mechi hiyo kuwa suluhu.

Na katika mechi nyingine iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka duniani katika kundi hilo B ni kati ya Ujerumani na Chile. Hata hivyo katika mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Krestovsky, timu hizo nazo zilitoka suluhu ya kufungana bao 1-1.

Alexis Sanchez alikuwa wa kwanza kuipatia bao la kuongoza kwa upande wa Chile ikiwa ni dakika ya 5, lakini naye Lars Stindl wa Ujerumani alisawazisha bao hilo kwenye dakika ya 41. Mpaka sasa Chile na Ujerumani ndio wanaongoza kundi hilo wakiwa na alama 4 kia mmoja wakifuatiwa na Australia na Cameroon wote wenye alama moja moja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents