Michezo

Confederations Cup 2017: Nivita ya Urusi na Ronaldo leo

Michuano ya kombe la mabara inatarajia kuendelea leo kwa kuzikutanisha timu za kundi A.

Katika mchezo wa kwanza unatarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Otkrytie Arena, wenyeji Urusi watavaana na Ureno huku Mexico ikicheza na New Zealanda kwenye mchezo wa pili katika uwanja wa Fisht Sochi.

Mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo( kushoto) akiwa na mchezaji wa Mexico mchezo ulio malizika kwa droo ya magoli 2 kwa 2

Wakati huo huo michezo ya kundi B inatarajiwa kuchezwa hapo kesho kwa kuzikutanisha muwakilishi wa Afrika timu ya taifa ya Cameroon itakapocheza na Australia na huku Ujerumani ikijitupa uwanjani kuvaana na Chile.

Mfumo wa video ulivyoleta sinto fahamu kwa wachezaji wa taifa ya Chile katika mchezo wao dhidi ya Cameroon

Michezo ya mwisho ya hatua hii inatarajiwa kufanyika Juni 24 ambapo mwenyeji Urusi itacheza na Mexico huku New Zealand ikicheza na Ureno.

Na katika michezo mingine ya mwisho ya kundi B itakayochezwa Juni 25, timu ya taifa ya Chile itakutana na Australia huku Cameroon wakicheza na Ujeruman ili kupata washindi watakao tinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

BY HAMZA FUMO 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents