Bongo Movie

Confirmed: Uwoya aamua kuachana na Bongo Movie, hataigiza tena

Mwigizaji maarufu wa Bongo movie Irene Uwoya amethibitisha uamuzi aliouchukua hivi karibuni wa kuachana na ulimwengu wa filamu ambao ndio umempa umaarufu na mafanikio aliyonayo katika miaka kadhaa iliyopita.

Irene

Uwoya ameachana na kuigiza lakini bado ataendelea kuonekana sana katika runinga kwasababu kilichomfanya mwigizaji huyo mrembo kuamua kuupa kisogo ulimwengu wa Bongo Movie ni fursa nyingine aliyoipata hivi karibuni ya kuanzisha kipindi kipya cha TV kiitwacho ‘PARADISE’ ambacho kimeanza kuonekana kupitia Clouds TV.

“Nimeamua kuacha mambo ya movie na kuwaachia wengine, haya maamuzi nimeyafanya kama miezi sita iliyopita… Mara ya mwisho kuigiza ni zaidi ya miezi sita iliyopita pia.”
Uwoya aliiambia DSTV.

Kipindi kipya cha Uwoya ‘Paradise’ ni kipindi chenye maudhui ya kusaidia watanzania kukarabati nyumba wanazoishi na kuzimiliki zinazohitaji kukarabatiwa na gharama zote za ukarabati kulipwa na ‘Paradise’.

Uwoya ambaye ni mama wa mtoto mmoja amewahi kupata tuzo ya mwigizaji bora kike 2012/2013 katika tuzo za Steps.

SOURCE: DSTV

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents