Habari

Congo: Kiongozi wa kivita wa kundi la ‘Mai-Mai Sheka’ ajisalimisha

Kiongozi wa kivita wa kundi la Mai-Mai Sheka, Ntabo Ntaberi, anayetuhumiwa kuhusika na kampeni kubwa ya ubakaji katika mji wa Walikale mwaka 2010 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC Jumatano hii amejisalimisha kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini humo.

Hati ya kukamatwa Ntabo Ntaberi ilitolewa mwaka 2011 na mahakama ya kijeshi ya DRC na tangu wakati huo alishutumiwa na mashirika ya haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na Human Rights Watch, kuua raia kadhaa.

Ntabo Ntaberi amejisalimisha katika eneo la Mutongo katika mji wa Walikale na kusafirishwa mjini Goma na Umoja wa Mataifa ambapo atazuiliwa kwa muda wa siku kadhaa, kwa uchunguzi wa afya kabla ya kukabidhiwa kwa serikali ya DRC Congo.

Shirika la kutetea haki za binaadamu lililoko mjini New York limetoa rai kwa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kumtendea mtuhumiwa huyo ubinaadamu wakati wote wa kesi yake na kwamba haki zake kama binaadamu zisikiukwe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents