Michezo

Conor McGregor apokea kipigo cha karne kutoka kwa Khabib ‘alitukana dini yangu, nilikuwa tayari kufa’ (+video)

Baada ya kukaa kimya kwa miaka miwili mfululizo kwenye mapambano ya UFC, Mwanamasumbwi Conor McGregor leo alfajiri amepokea kipigo cha mbwa koko kutoka kwa Mrusi Khabib Nurmagomedov.

Khabib  alikuwa anatetea mkanda wake wa Lightweight katika pambano hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa T-Mobile Arena jijini Las Vegas nchini Marekani.

Mrusi huyo anaendeleza rekodi yake ya ushindi na mpaka sasa amepigana mapambano 27 bila kupoteza hata moja. Pambano la leo ni pambano lake la kwanza kutetea mkanda wake baada ya kuuchukua toka kwa McGregor aliyevuliwa ubingwa baada ya kukaa nje kwa kipindi kirefu akijiandaa na pambano la ndondi dhidi ya Floyd Mayweather.

Hata hivyo, Khabib hakupewa mkanda huo jukwaani, hii ni baada ya vurugu kubwa kuibuka kwenye ukumbi huo jambo ambalo liliwalazimu walinzi na polisi kuingilia kati baada ya Khabib kuruka nje ya uwanja na kuivamia timu ya McGregor.

Khabib kwenye mkutano wake na waandishi wa habari baada ya pambano, aliomba radhi na amesema ushindi wake ulikuwa ni wa lazima kwani McGregor kabla ya kupigana alikuwa anatukana dini yake ya kiislamu jambo amabalo lilimkera sana.

Pambano la jana linatajwa kuwa ni pambano kubwa katika historia ya UFC, McGregor alikuwa na timu ya watu wengi nyuma yake akiwemo Drake ambaye alikuwa mpambe kwenye kila sehemu aliyokuwa McGregor.

https://youtu.be/1UM6XkLwppQ

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents