Conor McGregor atangaza kustaafu ngumi, Rais wa UFC Dana White na mashabiki wa MMA washtushwa na taarifa hizo
Conor McGregor ametangaza kustaafu kupambana kwenye mapambano ya UFC.
Bondia huyo wa MMA (21-4 MMA, 9-2 UFC) mwenye umri wa miaka 30, hata hivyo yupo kwenye adhabu baada ya kusababisha vurugu kwenye pambano la Nevada State Athletic Commission UFC 229 dhidi ya Khabib Nurmagomedov.
Kupitia akaunti yake ya Twitter, mpambanaji huyo anayetumia viungo vyote ndani ya ulingo maarufu kama ‘Mixed Martial Art’ ameandika ujumbe wa kustaafu kwake siku ya Jumanne na kuwashtua mashabiki wengi.
”Nimeamua leo hii kustaafu kucheza mchezo huu unaojulikana kama
‘Mixed Martial Art’, nawatakia wale wote wanafunzi wenzangu kuendelea na mashindano,” amesema McGregor.
Conor McGregor ameongeza ”Kwa sasa najiunga na washirika wenzangu ambao tayari walishastaafu.” alimalizia hivyo.
Kwa upande wake rais wa UFC, Dana White amekiri kushangazwa na taarifa hizo baada ya kupita saa moja tangu McGregor kutoa taarifa hiyo kupitia Twitter .
“Anazo fedha za kustaafu, na ana mvinyo,” amesema White huku akiongeza kupitia ujumbe wake. “Kabisa haishangazi, kama mimi ningekuwa ndiyo yeye ningetangaza kustaafu pia, anastaafu akitokea kwenye mapambano ninahakika kunakitu kingine anahitaji kuendelea nacho na ameshamaliza yale makubwa aliyotaka kufanya kwenye michezo.”