Michezo

Conor McGregory atokwa machozi mbele ya kadamnasi baada ya kumtwanga mpinzani wake ndani ya sekunde 40 (+Video)

Mkali wa MMA, Conor McGregory ameandika historia mpya katika maisha yake ya ulingoni baada ya kumpiga mpinzani wake, Donald Cerrone ndani ya sekunde 40 na kujikuta akibubujikwa na machozi mara baada ya ushindi huo.

https://www.youtube.com/watch?v=GzcLf_dvzR0

Katika pambano hilo lililomrudisha, Conor McGregory rasmi katika ulimwengu wa ‘Mixed martial arts’ (MMA) mchezo ambao unaruhusu kutumia viungo vyote vya mwili, ulimshuhudia bingwa huyo wa MMA akionyesha uwezo wa hali ya juu.

Conor McGregor ameshinda pambano dhidi ya Donald Cerrone kwa TKO raundi ya kwanza tu kunako sekunde ya 40. Pambano hilo lisilo la ubingwa limepigwa T-Mobile Arena huko Las Vegas. McGregor sasa ni bondia wa kwanza kushinda kwa KO kwenye uzito wa Featherweight, Lightweight na Welterweight.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents