Michezo

COPA AMERICA: Lionel Messi apigwa kadi nyekundu ya pili katika maisha yake ya soka, Agoma kuchukua medali ya mshindi wa tatu, Aeleza sababu

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina ambaye pia ndiye nahodha wa kikosi hicho, Lionel Messi jana usiku amepata kadi nyekundu ya pili katika maisha yake ya soka tangu mwaka 2005 alipopata kadi nyekundu ya kwanza.

Kwenye mchezo huo wa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano ya Copa America, Argentina walishinda goli 2-1 dhidi ya Chile na Lionel Messi hakuonekana jukwaani wakati wa kuchukua medali za mshindi wa tatu.

Akielezea sababu za kutochukua medali hiyo, Lionel Messi amesema kuwa ni masuala ya rushwa yaliyogubika michuano hiyo, Huku akieleza kuwa kuna baadhi ya timu tayari zimeshatangazwa ubingwa hata kabla ya kucheza.

Sijaenda kuchukua medali kwa sababu sitaki kuwa mmoja ya wala rushwa, Brazil watashinda mchezo wao wa fainali. Kwani fainali hiyo tayari imeshapangwa na ni muda tu ndio unaosubiriwa na mimi daima nitaendelea kuongea ukweli,“ameeleza Messi kwenye mahojiano yake na waandishi wa habari baada ya mchezo huo kumalizika.

Mwamuzi wa mchezo huo, Mario Diaz aliwapiga kadi nyekundu Lionel Messi na mwenzie Gary Medel baada ya kutunishiana misuli uwanjani, kitendo ambacho Messi hakukifurahia na akisisitiza kuwa ulikuwa ni muendelezo wa upendeleo unaofanywa na Shirikisho la Soka la Amerika Kusini CONMEBOL ambao pia ndio waandaaji wa michuano hiyo.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents