Afya

Corona tishio Marekani yasambaa kwa kasi majimbo 16, kwa siku maambukizi 40,173

Daktari mkuu wa magonjwa ya kuambukizwa nchini Marekani Dkt Anthony Fauci anasema Marekani ina tatizo kubwa kwa kuwa maambukizi ya virusi vya corona imepanda kwa kasi katika majimbo 16.

Ndani ya miezi miwili alitoa ufafanuzi mfupi kwa wahudumu wa White House,Dkt Fauci alisema: “Namna nzuri ambayo tunaweza kukabiliana na janga hili ni kwa kushirikiana pamoja.”

Kama mtaalamu wa afya alisema kuna mambo mengi ya kuyafanya ili kupunguza kasi ya maambukizi, makamu wa rais Mike Pence alisifia jitihada ambazo Marekani ilizichukua”.

Zaidi ya maambukizi mapya 40,000 yalipatikana nchini Marekani siku ya Ijumaa.

Jumla ya maambukizi 40,173, ambayo yalitolewa na chuo kikuu cha Johns Hopkins, ilikuwa idadi kubwa kwa siku mpaka hapo, na rekodi ya maambukizi ilizidi kwa siku moja tu.

 

Marekani kuna zaidi ya maambukizi milioni 2.4 yaliothibitishwa na vifo zaidi ya 125,000 katika nchi nzima – idadi ambayo iko juu kuliko nchi nyingine.

Katika taarifa fupi aliyotoa siku ya Ijumaa, kikosi kazi cha White House waliwahimiza vijana pia kupima hata kama hawaoni dalili.

Bwana Pence alisema rais amekitaka kikosi kazi cha operesheni hii kuwaeleza Wamarekani kuwa kuna maambukizi mengi na kuna wagonjwa wengi wamelazwa hospitali katika majimbo ya kusini na Magharibi.

Jimbo la Texas, Florida na Arizona, mpango wa kufungua shughuli ziendelee umesitishwa kwa sababu ya kasi ya maambukizi.

Wakati maeneo mengine kesi za maambukizi zikiwa zinaongezeka kila kukicha na hivyo kufanya rekodi ya walioambukizwa kuongezeka pia.

Maafisa wa afya wa Marekani wanakadiria kuwa idadi ya maambukizi yaweza kuwa imeongezeka mara kumi zaidi ya ripoti iliyotangazwa.

Walisema nini katika Ikulu ya Marekani?

Dkt Deborah Birx, mratibu wa kikosi cha kukabiliana na virusi vya corona, amewashukuru vijana wa Marekani kwa kuzingatia muongozo wa maofisa na kupima virusi hivyo/

“Badala ya kuwaambia wakae nyumbani, sasa hivi tunawaambia wakapime.”

Amegundua mabadiliko haya, anasema katika muongozo wa kupima utaweza kuwasaidia maofisa kuweza kubaini wale ambao wana maambukizi na wale wenye dalili ambazo hazijioneshi kwa haraka na mwanzoni hatukuweza kuzipata kabla”.

Dr Birx
Kufuatia takwimu ambazo Dkt.Birx aliwakilisha hivi karibuni , Dkt. Fauci alisema: “Kama mnavyoona tunakabiliana na tatizo kubwa sana katika baadhi ya maeneo.”

Aliongeza: ” Hivyo athari inayopatikana katika eneo moja la nchi inaweza kuathiri maeneo mengine vilevile.”

Dkt Fauci alisema ongezeko la maambukizi kwa sasa ni kutokana na kila kitu ambacho kinaendelea katika taifa hilo na inawezekana kufungua kwa wakati huu ni jambo la mapema sana hivyo kufungua katika wakati muafakandio jambo sahihi na wananchi wenyewe kufuata muongozo unaotolewa.

“Watu wanawaambukiza watu wengine na inapelekea kuwaambukiza watu ambao afya zao ni dhaifu kama wazee,” alisema.

“Inabidi kila mtu awe makini kwa ajili ya afya yake na jamii pia kwa sababu kama tunataka kumaliza mlipuko huu… lazima tufahamu kuwa sisi ni sehemu ya mapambano.”

Dkt Fauci aliongeza kusema kuwa kama maambukizi hayataisha , hata maeneo ya nchi ambayo yako vizuri yataathirika tu.

Aidha makamu wa rais alisifia jinsi taifa linavyokabiliana na mlipuko huo na kuainisha maeneo kama New York na New Jersey kuwa na maendeleo makubwa ya kupungua kwa maambukizi.

“Tumepunguza kasi ya maambukizi, tumeweza kuokoa maisha ya watu ,” alisema.

Bwana Pence alionekana kukanusha uhusiano wowote wa kufungua kwa baadhi ya majimbo na ongezeko la virusi vya corona.

Akijibu swali la mwandishi wa habari, alisema majimbo ya kusini ambayo yamefunguliwa miezi kadhaa iliyopita , wakati ambao kesi za maambukizi ikiwa chini.

Badala ya bwana Pence kulaumu zaidi katika upande wa ongezeko la maambukizi kutokana matokeo mengi ya vijana waliopima kuonyesha wana vipimo, na kuongeza kuwa labda wako kwenye hatari ndogo ya kupata dalili kubwa hivyo wanapaswa kuwa makini a kufuata ushauri unaotolewa na serikali.

Presentational grey line

Ni vigumu kukubali Matokeo

Uchambuzi

Ilikuwa ni wiki ngumu kwa White House.

Idadi ya maambukizi iliongezeka kwa kasi wakati magavana walivyokuwa wanajaribu kutekeleza ujumbe wa rais Trump kuwa taifa linarudi katika hali yake ya kawaida.

Ongezeko la maambukizi liliwashtua watu wengi na makamu wa rais bwna Pence alitoa salamu zake za rambirambi kwa wale waliopoteza ndugu zao.

Na kusifu utawala wa e Trump kwa kufanya jitihada nzuri za kukabiliana na ugonjwa huo.

Wakosoaji walikosoa maelezo yake kutokana na hali ilivyo mbaya.

Pence ana kazi ngumu ya kuanza kuunga mkono maamuzi yenye utata ya bwana Trump’.

Kile alichozungumza bwana Pence wengi hawakukiamini .

Bar staff check patrons' ID at Under the Volcano in Houston, Texas, on May 22, 2020
Presentational white spaceHali ni mbaya kiasi gani?

Mfumo wa serikali ya Marekani inaruhusu majimbo kuwa huru kufanya shughuli zao na kujilinda katika janga la kitaifa la kiafya.

Magavana ndio wana jukumu la kuondoa maruuku ya kutoka nje katika eneo husika lakini hali imekuwa ndivyo sivyo hata kama walikuwa na nia ya kufanya hivvyo.

Jimbo la Texas, ambalo lilikuwa mstari wa mbele katika mpango wa kuondoa amri ya kutotoka nje , sasa imeshuhudia maelfu ya maambukizi mapya na hivyo kufanya gavana wa Republican Greg Abbott kuamua kusitisha kufunga jimbo hilo siku ya Ijumaa.

Alitangaza kuwa klabu zote zifungwe na kutoa amri ya migahawa kufunguliwa kwa asilimia hamsini tu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents