Tia Kitu. Pata Vituuz!

CORONA VIRUS: DStv yapanua wigo wa habari, elimu na burudani kwa wateja wake

Ni katika jitihada za kuhakikisha jamii inapata habari za uhakika, elimu ya kutosha na burudani kipindi hiki cha mapambano dhidi ya corona

Pamoja na changamoto iliyopo duniani kwa sasa, MultiChoice inawahakikishia wateja wake wa DStv kuwa inayazingatia mahitaji yao hasa ukizingatia kuwa kwa sasa watu wengi wanalazimika kukaa nyumbani katika jitihada za kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

“Tutaendelea kukupa wigo mpana zaidi wa kupata habari za uhakika kwa kufungua chaneli za habari kwenye vifurushi vyetu.

Tunazingatia mawasiliano ya mara kwa mara na mamlaka husika na tutashiriki kikamilifu katika kupambana na kuenea kwa ugonjwa wa Covid-19. Ni muhimu sana sote tuzingatie maelekezo na maagizo yanayotolewa na mamlaka sahihi na wataalamu wetu ili kuhakikisha kuwa tunalinda afya zetu na za wenzetu” amesema Jacqueline Woiso, Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania

Mkurugenzi huyo ametangaza rasmi kwamba kuanzia sasa;

  • Fahamu kinachoendelea

Ili kukuwezesha kupata habari na taarifa za uhakika katika kipindi hiki, tunapanua wigo wa habari kwa kufungua chaneli kubwa za habari katika vifurushi vyetu. Kuanzia leo chaneli ya CNN (401) na Euronews (414) zitafunguliwa kwa wateja wa vifurushi vyote kuanzia kile cha chini kabisa cha DStv Bomba. Pia tumefungua chanel maarufu ya habari za Afrika Africanews (chaneli 417) kwenye vifurushi vyetu vyote hadi tarehe 1 Mei ambapo chaneli hii itakuwa inapatikana kuanzia kifurushi cha DStv Family.

  • Kwa watoto

Kwa kuzingatia kuwa Watoto wetu wako likizo kipindi hiki, maudhui ya elimu ya mezingatiwa ambapo chaneli ya elimu ya Da Vinci (Chaneli 318) na ile ya burudani ya Cartoon Network (channel 310) sasa zimefunguliwa kwa vifurushi vyote kuanzia cha chini kabisa cha DStv Bomba. Hii ni katika jitihada za kuhakikisha watoto wetu wanaendelea kupata elimu na burudani wakati huu wakiwa nyumbani.

  • Michezo

Kama unavyo fahamu, matangazo mubashara ya michezo mbalimbali yameathiriwa sana kwani michezo mingi sasa hivi imesitishwa.

Hata hivyo ili kuhakikisha kuwa hupungukiwi na burudani kipindi hiki ambacho unashauriwa kupunguza mizunguko na safari zisizo za lazima, tunakuletea Makala maalum za michezo (sport documentaries) kutoka kila pembe ya dunia pamoja na kuonyesha matukio makubwa ya kimichezo yaliyotokea siku za nyuma. Pia chaneli maarufu ya michezo SuperSport1 (201) sasa imefunguliwa katika kifurushi cha DStv Compact na DStv Compact Plus.

Chaneli hii itakuwa na matukio yaliyoweka rekodi katika ulingo wa michezo duniani. Kwa wale wapenzi wa mbio za magari wataburudika na chaneli ya SuperSport7 (207) ambayo imefunguliwa kwa vifurushi vyote.

Huduma kwa wateja: 

Tunajali afya za wateja na wafanyakazi wetu, katika kipindi hiki cha tahadhari tumeandaa utaratibu ambapo baadhi ya wafanyakazi watafanyakazi wakiwa nyumbani.

Hii inamaana kuwa kunaweza kukawa na kuchelewa kupata huduma. Hatahivyo tuna njia nyingi mbadala za kidijitali -kimtandao ambapo mteja anaweza kupata huduma nyingi kwa urahisi na ufanisi zaidi.

Huduma hizo ni pamoja na; My DStv App inayopatikana kwenye Google Play na App Store, IVR – huduma ya sauti iliyorekodiwa, Huduma ya WhatsApp kwa namba 0677 666 111 ambapo unaweza kufanya malipo, kubadili kifurushi, kuangalia salio na huduma nyingine muhimu. Pia unaweza kupiga simu Huduma kwa wateja kupitia namba +255 222 199600 na +255 784 104 700, Tovuti : www.dstv.com, USSD: *150*53# pamoja na huduma ya ujumbe mfupi SMS kwenda 15727

Kwa wewe unayetaka kufungiwa hudumaya DStv wakati huu, fahamu kuwa mafundi wetu wote wamechukua tahadhari kubwa kuhakikisha kuwa wanafanyakazi kwa usalama.

Mafundi wamepewa mahitaji muhimu na maelekezo rasmi ya kuchukua tahadhari wakati wa kutoa huduma.

Mabadilikoyaratiba

Kutokananahalihiiyadharura, michezomingiimeathirika. Atharihizi pia zimezikumba tasnia nyingine za michezo na burudani kama vile uzalishaji wa filamu.

Tutakuwa tukiwajuza wateja wetu kuhusu mabadiliko ya ratiba kadiri yatakavyo kuwa yanatokea. Pi unawezakutembelea www.dstv.com

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW