Habari

Corona yaanza kusambaa Afrika

Mamlaka ya Afya nchini Nigeria leo siku ya Ijumaa imeripoti kesi ya kwanza ya mtu mmoja kukutwa na virusi vya Corona jijini Lagos. Hii ikiwa ni kesi ya kwanza ya ugonjwa huo Kusini mwa Jangwa la Sahara. 

 

Nigeria inaungana na nchi nyingine nne ambazo kwa mara ya kwanza zina tangaza kesi ya ugonjwa huo ikiwemo New Zealand.  Mgonjwa huyo ni raia wa Italia anayefanya kazi ndani ya nchi hiyo ya Afrika.

Nigeria inakuwa Nchi ya tatu Afrika kupata mgonjwa wa corona baada ya Misri na Algeria.

Kiongozi Mkuu wa Matibabu nchini England ameonya kuwa ni swala la muda tu, hadi Virusi vya Corona kuenea UK, kwani idadi ya kesi hizo imezidi kukuwa na kufikia 16.

Watu watatu walikutwa na virusi vya Corona UK siku ya Alhamisi huku wakati kwa mara ya kwanza Northern Ireland ikitangaza kupatikana kwa kesi hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents