Michezo

Corona yapelekea Pogba atolewa ndani ya kikosi cha Ufaransa

Mchezaji wa Manchester United Paul Pogba amepatikana na virusi vya corona na hivyo kuenguliwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kwa mujibu wa Didier Deschamps.

Paul Pogba - Player profile 19/20 | Transfermarkt

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27, atahitajika kujitenga na wala hatoshiriki michezo kadhaa itakayopigwa na timu yake ya taifa ya Ufaransa.

Pogba huwenda akawa sehemu ya kikosi cha kwanza cha Man United kitakachoshuka dimbani Septemba 19 kuwakabili Crystal Palace ndani ya uwanja wa Old Trafford ikiwa ni mchezo wao wa kwanza wa ufunguzi wa Priemier League.

“Kila mmoja United anamtakia Paul afya njema kabla ya kuanza kwa msimu ujao.” Ujumbe kutoka ndani ya klabu ya Manchester United.

IMEANDIKWA NA HAMZA FUMO, INSTAGRAM @fumo255

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents