Burudani

Country Boy azitaja sababu zinazowakwamisha rappers wachanga

Country Boy amesema rapper vijana wana nafasi ya kufanya vizuri kimuziki lakini kinachowakwamisha ni kukosa msaada kutoka kwa wadau.

IMG_9455

Country Boy ameiambia bongo5 kuwa endapo wadau wataamua kuwasaidia rapper vijana muziki utaweza kwenda mbali zaidi.

“Young rapper tunaweza kuleta mabadiliko makubwa sana kwenye muziki wetu,” amesema. “Sisi hatuna majukumu ya kuwaza sana zaidi ya kuwaza kazi. Mimi naamini tunaweza endapo tukipata ile support ya kutosha kabisa itayotuwezesha kutoka hapa kwenda sehemu nyingine.”

“Mimi naamini rapper kama Young Dar es salaam, mimi, tukipewa nafasi tunaenda mbali zaidi. Kwa hapa Tanzania tunashukuru Mungu tunaonekana lakini bado hatujafika kwenye level tunayohitaji ili tuwe wakubwa zaidi. Kwa sababu muziki wa sasa hivi unahitaji budget nzuri kwenye kila kitu. Ukifanya low budget video huwezi kwenda kokote na hii itanatokana na kukosa support ambayo inaweza ikamfanya afanye video kubwa.”

Rapper huyo amesema anatarajia kutoa ngoma mpya iitwayo
‘Mtaa kwa Mtaa’ aliyomshirikisha G-Nako.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents