Burudani

Country Boy, Motra the Future watia neno ‘beef’ la Wakazi na Godzilla

Wasanii wa Hip Hop, Country Boy na Motra the Future wamesema ni vema wasanii wenzao Wakazi na Godzilla wakamaliza tofauti zao mapema au kuhakikisha tofauti hizo zinabaki kwenye muziki tu na sio kuingilia mambo mengine.

Rapper Country Boy amesema kitu wanachokifanya sio kibaya ila kinaweza kuwa kibaya kwa namna wanashughulika nacho kwani wananchi wanakipokea kwa picha tofauti.

“Mimi naona wanapeana vitu vizito kiasi kwamba vinaweza kumstress mtu mmoja au mwingine kutokana kwamba kila moja ana hasira zake, siwezi kujua ugomvi wao ulianzia wapi mpaka wakanza kupishana, kama ni beef mimi napenda ya musically. Nachohofia itaenda kufika hadi nyumbani halafu itakuwa mbaya kwa sababu huwezi kujua mtu ana mapokezi gani katika moyo wake kwa kile anachokisi,” amesema Country Boy.

“Mimi nashauri kama kweli wamedhamiria beef yao iwe hivyo, basi wai-control iwe ya music na wa-battle kwa ajili ya mistari tu kwa sababu wao ni kioo cha jamii, na mnapohamia katika upande wa pili watu wanawaangalia kwa kwa jicho la tatu,” ameongeza.

Kwa upande wake Motra the Future amesema kwa mtu asiyewajua wasanii hao anaweza kusema wanatafuta kiki kumbe sivyo na kushauri kuwa wajitadhimini kwani kuna wadogo zao katika muziki ambao wanatengemea kujifunza mengi kutoka kwao.

“Kwa the way mimi ninavyojua kwenye muziki wa hip hop wa kibongo mwisho wa siku wanaweza kufauatana mpaka manyumbani, kwa hiyo inabidi wafanye mpango hili suala liishe, halafu sisi wadogo zao tunawaangalia tunaona hawa mabroo ni vipi, wanafanya vitu ambavyo sisi tunatakiwa tuviige halafu wanafanya vitu vibaya,” Motra amekiambia kipindi cha Ladha 3600 cha E FM.

Ameongeza, “halafu ninavyoona sidhani kama kwenye mitandao ni sehemu ya kulumbani, kuna DM walumbanie kule, wakija huku waongee vizuri, kuna sisi wametu-inspire hadi kuingia kwenye game”.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents