Burudani

Video: Country Boy na kaka yake Babuu wa Kitaa kubattle kwenye ngoma mpya ‘Kigangsta Kisharobaro

Si Joh Makini na Nikki wa Pili pili pekee ambao ni mtu na kaka yake wanaofanya hip hop pamoja. Wengine ni Country Boy na hitmaker wa Kimbia na mtangazaji wa kipindi cha Bibi Bomba cha Clouds TV, Babuu wa Kitaa ambao hivi karibuni watasikika kwenye wimbo wa pamoja, ‘Kigangsta Kisharobaro’.

“(Babuu wa Kitaa) ni bro wangu kabisa, tumezaliwa watoto wanne, wa kwanza sister, wa pili sister, wa tatu Babuu, wa mwisho mimi,” Country Boy ameiambia Bongo5. Country Boy amesema kaka yake amemfundisha kusimama mwenyewe kwenye muziki bila kutegemea msaada wake, kitu ambacho anasema kimemsaidia.

2
Babuu wa Kitaa

“Bro wangu ana connection kubwa sana ya muziki, anajuana na watu wengi sana, mwisho wa siku alikuwa ananiambia kwamba ‘sikupeleki studio sikupeleki wapi, una muziki mzuri, una uwezo wa kuandika hustle mwenyewe, hangaika, sumbuka hata nauli sikupi’. Ngoma tumeshafanya bado kutoa tu mwaka huu ndio tunaiachia, tumeshafanya bonge moja la jiwe linaitwa ‘Kigangster Kisharobaro’. Yeye si anajifanya gangsta halafu mimi ananiita Sharobaro, nimemkazia mbaya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents