Burudani

Coyo amwaga sifa kwa Vanessa Mdee, ‘Natamani mke wangu awe kama yeye’

Msanii wa muziki Bongo, Coyo amemwaga sifa za kutosha kwa Vanessa Mdee kwa kile alichokiita ni msanii mzuri na anayejituma.

Coyo ambaye anafanya vizuri ngoma yake mpya ‘Nyakanyaka’ ameimbia The Playlist, Times Fm kutokana na jinsi Vanessa alivyo anatamani hata mke wake kuwa hivyo.

“Vee anaonekana ni mtu mwenye future ambayo ina mpangilio, kiufupi ni mwanamke ambaye anajituma kuanzia kwenye kazi zake na anajua ni kitu gani anakifanya, kwa hiyo huwa namkubali sana natamani sana hata wangu awe kama yeye lakini ila asiye na skendo kama za Gigy Money” amesema.

Kuhusiana na kumchana Gigy Money Coyo alisema ‘kitu kizuri kina kiki chenyewe siyo utafute kiki, kuna kitu kimekiki, kuna kitu kimetafuta kiki na kuna kitu kimetafutiwa kiki, hivyo ni vitu vitatu tofauti”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents