BurudaniUncategorized

Coyo athibitisha kuikosoa ‘Bongo Bahati Mbaya’ ya Young Dee

Msanii wa Bongo Flava, Coyo amethibitisha kuukosoa wimbo wa Young Dee kupitia ngoma yake mpya ‘ItakuCost’.

Kupitia ngoma yake hiyo kuna line inasema ‘chunga na maisha ya ku-act, kusema Bongo bahati mbaya’. Kupitia Times Fm amethibitisha ni kweli mstari huo ni kwa ajili ngoma ya Young Dee.

“Nimeongelea maisha ambayo yapo, kweli kuna watu ambao wanahisi wapo Bongo bahati mbaya wakati ukiangalia maisha yao halisi wanastahili kuwa Bongo,” amesema Coyo na kuongeza.

“Kuzaliwa Bongo Mungu kafanya makusudi sasa mtu anaposema Bahati mbaya anakuwa anakosea, huwezi ukatuigizia kisa tu umejulikana ndio unasema mimi Bongo bahati mbaya, si kweli wakati maisha yako chini tu kama kawaida,” amemaliza kwa kusema.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents