Burudani

Cpwaa afunika BBA

cpwaa2

Msanii Khalfan Ilunga ambaye anajulikana zaidi kama Cpwaa usiku wa kuamkia jana aliweka historia ya kuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania kupiga shoo katika fainali za Big Brother Amplified 2011.

 

Msanii huyo ambaye alipanda stejini majira ya saa mbili na nusu alipata nafasi ya kuimba nyimbo mbili za “So Pwaa” na “Action” aliowashirikisha msaanii Trinity, Dully Sykes pamoja na Ngwea.

Akiwa amevaa koti la rangi ya uzurungi na Tshirt yenye bendera ya Tanzania msanii Cpwaa alitambulishwa na Mtangazaji wa kituo cha Mnet Ik ambaye ndio alikuwa mwongoza shughuli katikausiku huo wa kuwakabidhi washindi tuzo zao.

Cpwaa hakuwaangusha mashabiki wake na moja kwa moja alijitokeza kwa mbwembwe na kulishambulia steji na kulakiwa kwa shangwe na mashabiki wa shindano hilo ambapo jana lilikuwa linafika Tamati.

Pamoja na Cpwaa wasanii wengine wa kiafrika waliopiga shoo ni pamoja na Wizkid, Amplified Crew, fally Ipupa

Fainali hiyo ilishuhudia mshiriki wa Nigeria Pamoja na wa Zimbabwe Wendel wakiondoka na pesa Taslim dola za kimarekani laki mbili mbili.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents