Burudani

Cpwaa atease nyimbo mbili mpya atakazoziachia kwa pamoja

Antoneyo na Cpwaa

Rapper na msanii aliyetajwa kuwania tuzo za CHOMVA2012, Cpwaa The Supreme leo (Nov 1) kupitia website yake ameweka vipande (snippet) vya ngoma zake mbili atakazoziachia kwa pamoja wiki ijayo.

Ngoma ya kwanza inaitwa Mission 12 O’Clock aliyowashirikisha Godzilla, Mabeste, Lord Eyez, One the Incredible na Antoneyo aka The Artist kutoka Marekani ambaye anafungua kwa verse moja kali. “When you go to work I go to sleep, when you go to sleep I go to work”, anasikika Cpwaa kwenye ngoma hii. Godzilla anafuata na kisha One anampokea kwa verse ya Kiingereza na kipande hiki kuishia hapo.

Isikilize kwa kufuata link hii

http://soundcloud.com/cpwaa-thesupreme/mission-12-oclock-cpwaa-ft-the

Track ya pili ambayo ina mahadhi tofauti kabisa na ya kwanza inaitwa ‘Mambo’ ambayo inamlazimu Mmarekani The Artist kutambaa vema kwenye beat hii ya kiafrika. Mwanzoni kunasikika acapella ambapo Cpwaa anamwambia Antoneyo, “welcome to Tanzania, East Afrika,the home of the greatest land, the swahili nation, the greatest women and the greatest culture” Kisha chorus inaingia kwa meneno, “ Niaje Do you speak English”!! nk.

Kwa uhakika hii ndio ngoma ambayo itafanya vizuri zaidi kuliko Mission 12 O’clock kutokana na kuwa na vitu vingi ambavyo ni kama fahari ya Afrika zaidi hasa pale Cpwaa anapotoa salamu kwa lugha mbalimbali kama kifaransa na kizulu. Ngoma hii imefanywa na producer Mona G wa Classic Sound.

Isikilize kwenye link hii

http://soundcloud.com/cpwaa-thesupreme/mambo-cpwaa-ft-antoneyo-the

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents