Michezo

CR7 ampiku Ronaldo pale Serie A, moto wake ni wa kuotea mbali, amuachia vumbi Batistuta

Nyota wa klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo amefikisha jumla ya mabao 50 ndani ya mechi 70 alizocheza tangu ajiunge na miamba hiyo ya soka ya Italia.

Image result for cr7

Mreno huyo alifikisha idadi hiyo ya magoli siku ya Jumapili baada timu yake kuifunga klabu ya Fiorentina kwa jumla mabao 3-0.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 35, anakuwa mchezaji wa pili katika ligi ya Serie A kufunga idadi hiyo ya magoli ndani ya michezo michahe akizidiwa na Andriy Shevchenko akitupia mabao 50 kwenye mechi 69 tu. Huku akimzidi Ronaldo raia wa Brazil aliyefunga magoli 50 kwenye mechi zake 77 alizoanza kucheza Seria A.

   1. ANDRIY SHEVCHENKO (magoli 50 mechi 69 tangu kuanza kukipigia Serie A)

Nyota huyu aliyekuwa akiitumikia AC Milan ndiye pekee aliyempiku Cristiano Ronaldo katika orodha hii  akifikisha idadi hiyo ya magoli kwenye michezo michache zaidi. Alifikisha idadi hiyo Januari 21, 2001 kwa kuwafunga Roma mabao 3 – 2.

   2. CRISTIANO RONALDO (magoli 50 mechi 70 tangu kuanza kukipigia Serie A)

Turudi kwa Cristiano sasa, baada ya kujiunga na Juventus msimu uliyopita, alifikisha idadi hiyo baada kuwafunga Fiorentina. Amekuwa akifunga mfululizo ndani ya michezo nane sasa ya Serie A.

   3. RONALDO (magoli 50 mechi 77 tangu kuanza kukipigia Serie A)

Kabla ya Cristiano, kulikuwepo na Ronaldo aliyekuwa akitinga jezi namba 9. Mbrazil alifikisha idadi hiyo ya magoli mwaka Octobea 2, 1999 kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Piacenza. Lakini alipotea haraka katika ramani ya soka kutokana na majeruhi yaliyokuwa yakimuandama.

Brazilian icon Ronaldo scored his 50th goal in Italian football for Inter against Piacenza in 1999

Inter ilitoa kiasi cha paundi milioni 13.2 na kuweka rekodi ya dunia kutoka Barcelona mwaka 1997, akiwa mchezaji kijana zaidi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia ‘FIFA World Player of the Year’.

  4. MARCO VAN BASTEN (magoli 50 mechi 83 tangu kuanza kukipigia Serie A)

Ilikuwa maajabu kwa legend huyu wa AC Milan kuchukua misimu mitatu kufikisha jumla mabao 50 mara tu baada ya kukanyaga ardhi hiyo ya Itali

Mdutch huyo alifikisha idadi hiyo kwenye mechi dhidi ya Cesana kunako Januari 7, 1990.

 5. MICHEL PLATINI (magoli 50 mechi 84 tangu kuanza kukipigia Serie A)

Fundi huyu wa Ufaransa alifikisha idadi hiyo katika msimu wake wa pili akiwa na Juventus, Februari 26, 1984.

 6. GABRIEL BATISTUTA (magoli 50 mechi 85 tangu kuanza kukipigia Serie A)

 7 .DAVID TREZEGUET (magoli 50 mechi 86 tangu kuanza kukipigia Serie A) ilifikisha idadi hiyo dhidi ya Chievo Verona, Januari 19, 2003.

 8. EDIN DZEKO (magoli 50 mechi 92 tangu kuanza kukipigia Serie A) aliifungia Roma, Agosti 26, 2017.

9. ADRIANO (magoli 50 mechi 95 tangu kuanza kukipigia Serie A)

10. GONZALO HIGUAIN (magoli 50 mechi 96 tangu kuanza kukipigia Serie A)

Muargentina huyo alifikisha idadi hiyo wakiwa anacheza Napoli, kwenye ushindi wa 4-2 dhidi ya Sampdoria mwaka 2015.

Imeandikwa na Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents