Habari

Crazy GK asema alirekodi ‘Baraka au Laana’ kufanya research

Msanii wa Hip Hop kutoka East Coast Team, Gwamaka Kaihula aka King crazy GK amefunguka kwa kusema wimbo wa Baraka au Laana haujamuumiza kwa kutofanya vizuri kwasababu alikuwa anafanya majaribio tu na amewataka wadau wasubiri ujio wake mwingine kabla ya mwaka kumalizika.

GK1

Akizungumza na Bongo5 leo, Crazy GK amesema muziki umebadilika na wasanii wa sasa wanafanya muziki kutokana na mahitaji ya soko wakati msanii anatakiwa afanye kile anachokifikiria kutoka kwenye hisia na sio kupelekeshwa na watu.

“Muziki wa sasa hivi unaburuza wasanii, unakuta wasanii wanafanya nyimbo kutokana na mahitaji wa watu. Wasanii hawaimbi vitu ambavyo vinatokana na hisia zao, wanaimba kwa kuangalia soko la muziki linataka nini. Wakati naona muziki utakuwa unapoteza ladha kwasababu wasanii wote tutaimba kitu kimoja kutokana mahitaji yao,” alisema GK.

“Nitaachia wimbo na video hivi karibuni ambayo itakuwa tofauti na ya kwanza. Sasa hivi mimi sio rapper tena kama akina Jay Z. Sasa hivi mimi ni mwanamuziki. Sasa hivi mimi napiga guitar na Kinanda kama nipo baharini naweza kuogelea mpaka kupiga mbizi. Hip Hop ipo so limited, yaani inamilikiwa kwahiyo ndio maana nikaenda chuo cha muziki kupata maujanja. Watu watakuwa wanashangaa umefanyaje umefanyaje hapo ila ndio maujanja hayo.East Coast team itakuwa na na nyimbo mbili na mimi ninazo zangu ila itatoKa video kabla ya mwaka huu kumalizika,” aliongeza.

Wakati huo huo GK amesema alikuwa nje ya game kwa muda mrefu kutokana na masomo ambako amesema amejifunza mengi sana.

“Unajua nimekuwa nje ya game kwa miaka kama mitano sasa, unajua hata kama mchezaji hajacheza kwa muda mrefu akiingia uwanjani utaona utofauti. Kwahiyo ni kama mimi. Kama nilikuwa jembe wakati ule sasa hivi nimekuwa TreKta, nimekuja na maujanja zaidi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents