Burudani

Crazy Moment: Pale nywele za Beyonce ziliponasa kwenye feni ya jukwaani (Video)

Hii inaitwa ajali kazini, just imagine (kama msanii wa kike) mbele ya umati mkubwa wa watu waliofika ukumbini kutazama show yako na wakiwa na shangwe za kutosha mara unashangaa nywele zako zimenasa kwenye ‘panga boy’ feni moja isiyo na adabu ya ukumbini hapo, hivi aliyeituma (hiyo feni) anajua umetumia masaa mangapi salon na umelipa shilingi ngapi? Na je anajua umeweka pozi ngapi kupiga picha za kuweka instagram kwa fans wako walio comment kukupa hongera umependeza nywele zako? LOL!! pole sana Beyonce maana huo mkanda wote umemtokea yeye. Picha kamili ingia ndani

Bey bey

Jumatatu usiku (July 22) Beyonce alikuwa na show huko Montreal, Canada wakati anaimba wimbo wake wa ‘Hallo’ ghafla si nywele zake zikanaswa na feni iliyokuwa nyuma yake jukwaani hapo, nina uhakika kwa msanii mwingine angeweza hata kupoteza mwelekeo na huenda ingemharibia show, lakini uzoefu na kujiamini vilimsaidia Bey mama wa mtoto mmoja (Blue Ivy) ambaye hakutetereka na aliendelea kuimba bila hata kupoteza mstari wala kutoka nje ya beat (Ki professional zaidi). Bey alisimama kwa muda huku wasaidizi wake wakijaribu kukata sehemu ndogo ya nywele zake na mkasi ili aweze kuwa huru na kuendelea na show. Zoezi lilifanikiwa na kipenzi cha Jigga aliendeleza makamuzi.

Baada ya show hiyo Queen Bey (31) aliwaandikia mashabiki wake kile kilichotokea lakini katika hali ya utani zaidi. Kama ilivyokawaida yake Bey hupenda kuandika kwa mkono mkono na hiki ndicho alichoandika na kuki post Instagram “Gravity can’t begiiiiin to pull me out of the fan again. I felt my hair was yankiiiin from the fan that’s always hatiiiiin. Virgin remy and Malaysiiiiiaaaaaan. Haaaaaa, I got snatched “2 snaps.” Goodnight,”.

Beyonce-note-

Tazama video ya tukio hilo

http://youtu.be/rKd9pOTJwL4

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents