AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Crazy World: Mwizi apitiwa usingizi kwenye sofa la nyumba aliyoingia kuiba!

Katika hali ya kuchekesha japo sio jambo la kucheka, mwizi mmoja alikamatwa na polisi wa Florida Marekani baada ya kukutwa amepiga usingizi kwenye sofa la nyumba alioingia kuiba, na kukutwa na vidani vya mmiliki wa nyumba aliovamia.

Pinkard--Domonique-jpg
Domonique Pinkard

Domonique Pinkard, (21) ndiye mtuhumiwa wa tukio hilo ambaye alikutwa na mwenye nyumba akiwa amelala usingizi kwenye sofa sebuleni huku mfukoni akiwa na vidani alivyokuwa ameiba tayari kwa kuondoka navyo.

Mwenye nyumba hiyo baada ya kumkuta mtuhumiwa akiwa amejiachia kwenye sofa lake kama kwake alipiga simu polisi, ambao baada ya kufika eneo la tukio walisema Pinkard alikuwa na mwenzake Julian Evangelist ambao walivunja mlango wa nyuma na kuingia ndani majira ya 7.30 a.m.

Waliendelea kusema Pinkard alijipumzisha kidogo kwenye sofa huku mwenzie akibeba TV na kusepa bila kumwamsha mwenzie.

Wapelelezi hao walisema Pinkard aliwaambia alikuwa amechoka na kazi ya kutwa nzima hivyo aliamua kupumzika kidogo ndipo akapitiwa na usingizi. Kwa mujibu wa WESH.

Polisi pia wamesema walikuta vidani vya mwenye nyumba vyenye thamani inayokadiriwa kufikia $500 katika mifuko ya Pinkard, kwa mujibu wa NBC Miami.Vitu vingine kama nguo na vifaa vya electronic vilikutwa nyumbani kwa mtuhumiwa wa pili Evangelist.

Watuhumiwa wote wawili walikamatwa na kufungwa kwa kosa hilo.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW