BurudaniUmbeaVideos

Chris Brown apora simu ya shabiki wake! [Video]


Msanii wa RNB Chris Breezy amekumbwa na balaa lingine linaloweza kumfanya akajikuta kafungwa jela. Breezy amekumbwa na madai ya umpora shabiki wake simu yake ya mkononi alipokua anatoka kwenye ukumbi wa starehe huko Miami, Florida.


Tukio hilo lilitokea usiku wa kumakia Jumapili tarehe 19 Februari, ambapo shabiki huyo anayeenda kwa jina la Christal Spann anadai kukutana na Breezy akiwa na rapper wa Young Money, Tyga, wakiwa wanatokea mlango wa nyuma wa club hiyo, alipochukua simu yake ya iPhone kumpiga msanii huyo picha, ambaye alimnyang’anya simu iyo na punde kusepa nayo katika gari Tyga alilokua anaendesha.

[embeded: src=”http://cdnapi.kaltura.com/index.php/kwidget/wid/1_pwd9b0zu/uiconf_id/6740162″ width=”560″ height=”340″ ]

Chris amekanusha madai haya na kudai ni hatua tu za kumchafua jina lake.

Tuhuma hizi zinaweza kumfunga Chris Brown hasa kwa sababu aliachiwa kwa onyo kali la kutokujihusisha na kitu chochote cha uvunjifu wa sheria baada ya kumtwanga demu wake wa wakati huo, Rihanna.

Cha kushangaza, Camp ya Riri inasema msanii huyo amesikitishwa na tuhuma hizo na ameamua kumpa ex wake support asilimia 200, na ameahidi kuwepo naye kumpa tafu no matter what!

Polisi wamesema wanaanzisha uchunguzi kwenye suala hili na wataoa statement baada ya kukamilisha.

Tusubiri tuyaone yatakayojiri!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents