Michezo

Cristiano Ronaldo apata mtoto wa nne

By  | 

Mchezaji bora wa dunia kutoka Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameongeza mtoto wanne katika familia yake.

Ronaldo amefanikiwa kupata mtoto huyo kupitia kwa mpenzi wake ambaye ni mwanamitindo wa nchini Hispania, Georgina Rodriguez.

Kupitia mtandao wa Instagram, mchezaji huyo ameandika jina la mtoto huyo ni Alana Martina.

Watoto wengine wa mchezaji huyo ni Cristiano Ronaldo Jr mwenye miaka saba na mapacha wake aliwapata mwaka huu Eva Maria na Mateo ambao mama yao bado hajafahamika.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments