Cristiano Ronaldo kutua Juventus kwa dau la pauni mil 88

Klabu ya Juventus ya nchini Itali inakaribia kunasa saini ya mshambuliaji wa Real Madrid na mchezaji bora duniani kwa sasa, Cristiano Ronaldo.

Kwa mujibu wa kipindi cha TV kinachorushwa nchini Hispania kinacho julikana kwa jina la Jugones kimeripoti kuwa Real Madrid ipo tayari kupokea kitita cha euro  milioni 100 sawa na pauni milioni 88 kutoka kwa Juventus ili kumuuza, Cristiano Ronaldo.

Television hiyo ya Hispania inayopatikana kwenye ‘station’ ya La Sexta imesema kuwa mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 33 ataridhia kuondoka baada ya kuwa  Bernabeu kwa miaka tisa.

Endapo dili hilo likikamilika Ronaldo atakuwa akikosunya kitita cha euro milioni 30 ikiwa sawa na pauni milioni 27 kwa mwaka. Inaaelezwa kuwa Madrid ipo tayari kupokea kitita hicho ili kumsajili mshambuliaji wa Brazil, Neymar.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW