Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Cristiano Ronaldo kuyaanika maisha yake ya ndani na nje ya uwanja kupitia mtandao wa Facebook

Licha ya timu yake ya taifa ya Ureno kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Dunia, mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amepata dili la mamilioni kupitia mtandao wa Facebook.

Image result for cristiano ronaldo
Cristiano Ronaldo

 

Dili hilo ni kwamba Ronaldo na familia yake wataandaa Reality Show yao ambayo itarushwa kwenye mtandao wa Facebook.

Kwa mujibu wa mtandao wa Variety umeeleza kuwa Facebook wapo kwenye mazungumzo na Ronaldo kuhusu kipindi hicho na imeelezwa tayari wametenga dau la dola milioni $10 sawa na tsh bilioni 22 za kumlipa mchezaji huyo bora wa dunia kwa mwaka 2017.

Kipindi hicho kitahusu maisha halisi ya Cristiano Ronaldo ndani na nje ya Uwanja ambapo mchumba wake Georgina Rodriguez na familia yake itahusishwa kwenye Reality Show hiyo.

Reality Show hiyo itakuwa na Episode 13 na itaoneshwa kupitia mtandao wa Facebook  kwenye sehemu ya Facebook Watch .

Hata hivyo, bado haijaelezwa ni lini Reality Show hiyo itaanza kurushwa, lakini kipindi hicho tayari kinasubiriwa kwa hamu na mashabiki wake.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW