Michezo
Crystal Palace yaiaibisha Chelsea EPL
Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Uingereza klabu ya Chelsea imekubali kipigo cha mabao 2-1 mbele ya Crystal Palace mchezo uliyochezwa hii leo.
Chelsea ambayo ilikuwa ugenini imekubali kipigo hicho kutoka Palace kupitia kwa beki Cesar Azpilicueta ambaye kajifunga na Wilfried Zaha huku la Chelsea likifungwa na Tiemoue Bakayoko.