Michezo

Crystal Palace yamtimua kocha wake baada ya kuiongoza michezo 5 pekee

Klabu ya Crystal Palace inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza imemuachisha kazi kocha wake, Frank De Boer baada ya kukiongoza kikosi hiko katika michezo mitano na siku 77 pekee.

The Eagles wapo nafasi ya 19 katika msimamo wa ligi ya nchini Uingereza baada ya hapo jana kulazimishwa kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Burnley huku kikosi hicho kikiwa chini ya De Boer kimeshindwa kushinda bao lolote katika michezo yake minne ya ligi.

Nafasi ya kocha huyo sasa inatarajiwa kuchukuliwa na aliyekuwa Meneja wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson.

Taarifa kupitia mtandao wa klabu hiyo umesema kuwa  wanamshukuru Frank kwa ushirikiano wake katika kipindi chote alichokuwa mahala hapo.

Meneja huyo wa zamani wa Ajax,De Boer alichukua kandarasi hiyo ya kuinoa Crystal Palace mwanzoni mwa msimu huu kwa kurithi mikoba ya Sam Allardyce aliyeisaidia timu hiyo kutoshuka daraja.

Frank De Boer alishawahi kuachishwa kazi katika klabu ya Inter Milan mwezi Novemba mwaka 2016 baada ya kuwa katika timu hiyo siku 85.

Na hii ni rekodi ya kocha De Boer katika timu alizopitia.

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents