Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Crystal Palace yathibitisha kumsaini kocha Roy Hodgson

Klabu ya Crystal Palace ya Uingereza imethibitisha kumteua, Roy Hodgson kuwa Meneja mpya wa timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili.

Meneja huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, Hodgson anatarajia kurithi mikoba ya Frank de Boer ambaye ametimuliwa katika kikosi hicho cha the Eagles na kumleta Ray Lewington kuwa msaidizi.

Hodgson mwenye umri wa miaka 70 anachukua nafasi hiyo ili kuiokoa Palace yenye matokeo mabovu katika ligi kuu nchini Uingereza baada ya kucheza michezo yake minne ya ufunguzi pasipo ushindi.

Hodgson, amesema kuwa “Hiyo ni timu ya ujanani mwake na amekuwa akifuatilia mara kwa mara pindi inapocheza jambo ambalo linampa nafasi ya kukumbuka mambo mengi”, ameuwambia mtandao wa klabu hiyo.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW