Habari

CUF ‘wazichapa’ Mahakama Kuu, wapewa onyo kali

Wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaomuunga mkono Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama, Prof. Ibrahim Lipumba na wanaomuunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif, nusuru wapigane Mahakama Kuu ya Tanzania leo katika wa kesi ya wabunge nane waliotimuliwa Uanachama CUF.

Wabunge wanane wa CUF waliovuliwa uanachama Prof. Lipumba walifungua kesi inayosikilizwa na Jaji Lugano Mwandambo, ambapo wabunge hao waliiomba Mahakama hiyo kuweka zuio la wabunge wapya kuapishwa hadi kesi ya msingi waliyofungua itakapoamuliwa.

Hata hivyo walipewa onyo kali ya kuiheshimu Mahakama na  polisi waliokuwepo eneo hilo hivyo sekeseke la vurugu hizo kumalizika na kila mtu kuwa tayari kusikiliza kesi hiyo.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents