Habari

CUF ya Profesa Lipumba yawavua uanachama wabunge 8 ‘wasaliti’

Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama cha Wananchi (CUF) limewavua uanachama wabunge 8 wa chama hicho kwa madai ya utovu wa nidhamu, ikiwemo kukisaliti chama hicho.

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba wa pili kutoka kulia

Mwenyekiti wa CUF, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba amesema, baraza pia limewavua uanachama madiwani wawili wa viti maalumu mkoani Dar es Salaam, kwa makosa kama hayo hayo.

“Leo asubuhi tumewasilisha nyaraka za hatua hizi kwa Spika na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa hatua zaidi,” amesema Profesa Lipumba mbele ya Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam.

Wabunge 10 wa CUF wanaomuunga mkono Seif Hamad wasusia kikao

Profesa Lipumba amesema wabunge hao wanane ni kati ya 10 walioitwa hivi karibuni na Kamati ya Maadili na Nidhamu kwa mahojiano wakitakiwa kujibu tuhuma zinazowakabili za kukihujumu chama hicho kwa maelezo kuwa walitaka kushirikiana na CHADEMA kumwondoa yeye madarakani.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents