Soka saa 24!

Cyrill Kamikaze afiwa na mama yake

Pasaka haikuja vizuri kwa rapper Cyrill aka Kamikaze. Rapper huyo wa kundi la Wakacha amempoteza mama yake weekend hii.

Cyrill alikuwa karibu mno na mama yake kiasi cha kumchukulia kama partner wake kibiashara.

Msiba huo umemsababisha muigizaji wa filamu na muimbaji Hemedy kuahirisha kuachia wimbo wake mpya leo ili kuomboleza kifo cha mama yake na mshkaje wake huyo wa karibu.

“Nasikitika kushindwa kuachia wimbo wangu mpya leo sababu ya msiba wa mama wa msanii rafiki kwangu cyril!!tukimaliza msiba nitafanya hivyo,” ametweet Hemedy.

Kwa mujibu wa Hemedy ibada ya kumuaga marehemu itakua leo saa 7 mchana na mazishi ni saa 9 alasiri katika makaburi ya Kinondoni.

Bongo5 inampa pole Cyrill kwa kumpoteza mama yake.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW